Mtoto akiwa amelala ndani ya Box lenye sakafu ya Makaratasi |
Kwa miaka 75, kina mama
wajawazito wamekuwa wakipewa na serikali visanduku vya karatasi. Visanduku
hivyo vimekuwa vikitolewa kama sehemu ya vitu muhimu vya mwanzo kwa mtoto
atakapozaliwa, kama vile vile nguo, mashuka na midori, ambavyo pia vinaweza
kutumika kama kitanda. Na baadhi ya watu wanasema vitu hivyo vimeisaidia
Finland kufanikiwa kuwa moja ya nchi ambayo ina viwango vya chini kabisa vya
vifo vya watoto duniani.
Imekuwa ni desturi
iliyojengekea ambapo visanduku vya karatasi hutolewa kwa mama wajawazito tangu
miaka ya 1930 na imepangwa na serikali kutolewa kwa watoto wote nchini Finland,
bila kujali hali ya familia wanazotoka, ni mwanzo wenye usawa katika maisha ya
watoto.
Godoro likiwa ndani ya
kisanduku cha karatasi linakuwa kitanda cha kwanza cha mtoto. Watoto wengi
kutoka familia zenye hali tofauti za maisha, kwanza wanalala katika sanduku
salama la karatasi la pembe nne.Vifaa hivyo ni pamoja na nguo za mtoto, mfuko
wa kulalia, vifaa vya kumbebea nje ya nyumba, sabuni za kuogea na mafuta ya
mtoto, pamoja na nepi, matandiko na godoro dogo.
Mpango wa mwaka 1947 wa vifaa
kwa mama mzazi, unampa chaguo la kuchukua sanduku hilo au kuchukua ruzuku ya
fedha taslimu, ambayo kwa sasa ni euro 140, lakini asilimia 95% wanapendelea
kuchukua sanduku ambalo lina thamani zaidi.
Utamaduni huuu umedumu tangu
mwaka 1938. Kwa kuanzia, mpango huu uliwahusu tu familia zenye vipato vya
chini, lakini ukabadilika mwaka 1949.
"Si tu kwamba uliwalenga
wanawake wanaotarajia kujifungua lakini sheria mpya ilimaanisha, ili kupata
ruzuku hiyo, au sanduku la mzazi, walitakiwa kumwona daktari au muuguzi wa
zahanati ya manispaa kabla ya kufikisha miezi minne ya ujauzito," anasema
Heidi Liesivesi, ambaye anafanya kazi Kela - Taasisi ya Bima ya Jamii ya
Finland.
Kwa hiyo sanduku hilo linakuwa
na vitu muhimu ambavyo mama wazazi wanatakiwa kuwa navyo kwa ajili ya watoto
wao wachanga, lakini pia inasaidia wanawake wajawazito kuwa katika uangalizi wa
madaktari na wauguzi wa serikali ya Finland.
Katika miaka ya 1930 Finland
ilikuwa nchi maskini na kiwango cha vifo vya watoto kilikuwa cha juu ambapo
katika kila watoto 1,000 waliozaliwa, 65 walifariki dunia. Lakini hali hiyo
ilibadilika haraka katika miongo iliyofuata.
Mika Gissler, profesa katika
Taasisi ya Taifa ya Afya na Ustawi mjini Helsinki, anatoa sababu kadha kuhusu
hili- sanduku la uzazi na huduma za kabla ya uzazi kwa wanawake katika miaka ya
1940, ikifuatiwa na mfumo wa Bima ya Afya ya Taifa katika miaka ya 1960 na
mtandao wa hospitali kuu.
Source BBC
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako