Thursday 6 June 2013

Dully Sykes apata msala kwenye msiba wa Ngwea Moro











MSANII wa kizazi kipya Dully sykes maarufu kwa jina la Mr misifa akutana na misukosuko wakati akitaka kuingia na gari lake katika uwanja wa Jamhuri sehemu ambayo mwili wa marehemu Albert  Mangwea uliagwa kabla ya kupumzishwa katika nyumba yake ya milele.

Sekeseke hilo lilitokea mara baada ya askari wa barabarani(traffic police) kumzuia dully sykes asiingie na gari lake ila apite mwenyewe  kwa kuhofia nafasi ya kuegesha magari  ila msanii huyo aligoma na kuamua kuwasha gari lake na kuondoka eneo hilo.

PATA PICHA iliongea na mtu wa karibu wa msanii huyo (Mr Blue)_ ambaye alisema Dully alikasirishwa na tukio hilo na kuona kuwa hakuthaminiwa kama wengine walioingia na magari yao. Ambapo baadhi wasanii waliingia na magari yao
PATA PICHA imefanikiwa kunasa  na kupata picha ya tukio hilo.

Danta, Failasufa na Von gasper

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako