Sunday 16 June 2013

DAMU YAMWAGIKA TENA ARUSHA


Watu wawili inasadikiwa wamefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa kutokana na bomu linalosadikiwa kutupwa kwa mkono Majira ya saa kumi na moja eneo la Soweto kata ya kaloleni mkoani Arusha.
Tukio hilo limetokea wakati chama cha demokrasia na maendeleo (chadema) kikifunga kampeni za udiwani katika uwanja wa kikapu uliopo Soweto. 
Katika tukio hilo raia walijikuta wakiingiwa na jazba na kuvunja kioo cha gari la kubebea wagonjwa kwa kile walichodai kuchelewa kuwahi kuwachukua majeruhi waliokuwa katika hali mbaya.
Katika kutuliza tafrani hiyo iliwalazimu polisi kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya raia walipandwa na jazba kufuatia tukio hilo, ambapo viongozi wa chama hicho Freeman Mbowe pamoja na Godbless Lema waliwasili eneo hilo baada tu ya tarifa ya mlipuko huo.

Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha chanzo cha mlipuko bado hakijafahamika hadi uchunguzi utakapofanyika.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako