Monday 10 June 2013

MAPACHA WENYE KILO NYINGI ZAIDI


Mapacha wanaojulikana kwa majina ya  Billy Leon McCrary na Benny Loyd McCrary waliozaliwa siku moja (December 7, 1946 )  ndio mapacha wanaoshikilia rekodi ya kuwa mapacha wenye uzito mkubwa zaidi tangu kuumbwa kwa Dunia, Benny Loyd McCrary akiwa na uzito wa kilogram 338 na Billy Leon McCrary kilogram 328.
Mapacha hao waliozaliwa katika jimbo la Hendersonville, North CarolinaUnited nchini America walianza kupata umaarufu baada ya kujiingiza katika michezo ya mieleka haswa wakiwa wanatumia jina la McGuire.
Unaweza kujiuliza je mapacha hawa kwa sasa hivi wanafanya shughuli gani au bado wanaendelea kucheza mieleka?,
 
Ukweli ni kwamba pacha anayejulikana kwa jina la Billy McCrary amefariki mnamo  july 14, 1979, akiwa na umri wa miaka 32, kwa ajali ya pikipiki, wakati pacha mwenzake anayejulikana kwa jina la Benny alifariki
miaka 21, baada ya kifo cha pacha mwenzake akiwa na miaka 54.kwa ugonjwa wa moyo kushindwa nguvu.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako