Friday 7 June 2013

SAFARI YA BAINES,FELLAINI KWENDA UNITED UTATA MTUPU.



 
Leighton Baines akifanya vitu vyake na jezi ya uingereza



MWENYEKITI wa klabu ya Everton Bill Kenwright amemuonya kocha mpya wa Manchester United David Moyes asahau wazo la kumfanya Leighton Baines kuwa Mchezaji wa kwanza kumsajili kutoka Everton.

Hatua hiyo imekuja baada ya Moyes kutaka kumfanya beki huyo wa Everton kuwa mrisi wa Patrice evra ndani ya kikosi cha manchester united.

Ken wright alisema Baines bado ana mkataba na timu hiyo na wanataka kuendelea kumtumia hivyo kumuongezea mkataba ndicho wanachokifikiria zaidi.

Mkurugenzi huyo amesema tayari wameshaanzisha mazungumzo na beki huyo wa kushoto wa uingereza juu ya kumuongezea wa miaka miwili ili aendelee kukipiga  ndani ya kikosi hicho.


Mwenyekiti huyo pia Bado ana imani ya kumbakisha ndani ya kikosi kiungo mahiri wa timu hiyo Marouane Fellaini katika mkataba wake na Everton kuna kifungu kinachomruhusu kusajiliwa na timu inayomtaka kwa dau la paundi million 24.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako