kikosi cha Timu ya taifa ya Tanzania Taaifa stars |
TIMU ya soka ya Tanzania imeshindwa kutamba mbele ya miamba
ya Afica ya kaskazini Morocco kwa kufungwa magoli 2-1, Katika mchezo mulioanza
majira ya saa tano kwa saa za Africa Mashariki.
Dakika ya 18, almanusura Thomas ulimwengu aipatie bao Stars mara
baada ya kuaambaa amba na mpira akipokea
pasi ndefu kutoka kwa nyota wa mchezo kwa upande wa stars Amri Kiemba lakini Ulimwengu alipioga
shuti mtoto lililodakwa na golikipa wa Morocco.
Moroccco walipata goli
kwa penati dakika ya 28 kufuatia beki
wa timu ya taifa ya Tanzania Agrey Moris kumsukuma mshambuliaji wa Morocco
aliyekuwa amebaki yeye na mlinda mlango wa Tanzania Juma Kaseja na kupelekea
kuzaa goli la kwanza lililodumu hadi mapunziko.
Kama hiyo haitoshi Mwamuzi wa mchezo huo alimzawadia kadi
nyekund mlinzi huyo na kufanya Stars kucheza wakiwa pungufu kwa karibia muda
wote.
Goli la Taia stars lilikwamishwa kimiani na kiungo Amri
Kiemba kwa shuti kali la umbali wa zaidi ya mita 30
Katika mchezo huo stars ilifanya mabadiliko kwa kumtoa
Mrisho Ngassa na Nafasi Yake Kuchukuliwa Na Nadir Haroub Canavaro kuziba pengo
la Moris aliyetolewa kwa kadi nyekundu, na Thomas ulimwengu nasi yake
kuchukuliwa na Hamis Mcha.
John Bocco "Adebayo" aliiingia mnamo dakika ya 95 akichukua
naasi ya Hamis Mcha aliyeonekana kupotea mchezoni.
FAILASUFA & DOX DANTA
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako