Monday 24 June 2013

AFYA YA NELSON MANDELA BADO HAIJAIMARIKA.

NELSON MANDELA



Jopo la madaktari wanaomtibu aliyekuwa rais wa zamani wa Afrika kusini,Nelson Mandela wamesema hali ya afya yake bado haijatengemaa.
Habari hizo zimekuja kupitia taarifa iliyotolewa na ofisi ya rais ya Afrika Kusini.
Taarifa hiyo imesema kuwa Mzee Mandela ameendelea kubakia hospitalini mjini Pretoria kwa siku ya kumi na sita akitibiwa mapafu yaliyosababisha tatizo kwenye mfumo wake wa upumuaji.
Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amemtembelea Mzee Mandela jumapili jioni na kuzungumza na jopo la matatibu wanaomtibia.Zuma pia amewaomba watu wote kumuombea Mzee huyo afya yake iimarike.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako