Thursday 13 June 2013

MSANII LANGA AFARIKI DUNIA

Msanii wa HIPHOP Langa (Lyrical and Natural Gifted Africa) enzi za uhai wake

Habari zilizotufikia hivi punde kutoka kwa watu wa karibu wa msanii LANGA KILEO kuwa, amefariki dunia Mida ya saa 11 jioni kwa ugonjwa wa Malaria alipokuwa amelazwa takribani siku tatu katika Hospital ya Muhimbili.
Afisa wUhusiano wa Hospital ya Muhimbili amethibitha habari hizo.

Msanii Langa alitamba baada ya kuibuliwa na Cocacola Pop stars akiwa na Witness, Shaa kwenye kundi lililopewa jina la WAKILISHA.
Alianza kufanya kazi zake peke yake mbali na kundi ambapo alitoa vibao mbalimbali ikiwemo Matawi ya Juu na Gangster.
MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU LANGA

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako