Kama ulidhani Manchester City na Chelsea ndio wanaofanya jeuri kwa kusajili
wachezaji bomba kwa ajili ya kikosi chao kwa msimu wa mwaka 2013-2014 basi
utakuwa umejidanganya kwani, katika kuhakikisha anaimarisha kikosi chake cha
Manchester United kocha mpya aliyekwaa kibarua hicho hivi karibuni na huyu si
mwingine bali ni David Moyes amekubali kutoa dau la paundi milioni 17 kumsajili
beki wa timu ya Benfica Ezequiel Garay.
Mchezaji huyo aliyesajiliwa na Manchester United ili kuboresha safu yake ya
ulinzi anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na kocha David Moyes tangu aajiliwe
rasmi kuwa kocha mpya wa Manchester united kurithi mikoba ya Sir Alex Ferguson
Ezequiel Garay. anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Manchester United
msimu huu baada ya Guillermo Valera mwenye umri wa miaka 20.
Wachambuzi wa masuala ya soka wanaoliona suala la Kocha David Moyes kusajili
mabeki hawa wawili ni kwa ajili ya kuja kuridhi mikoba ya Rio Ferdinand anayekaribia
kufikisha miaka 35 hivi karibuni na Nemanja Vidic, Chris smalling na Phil Jones
ambao hawaeleweki kutokana na kukumbwa na majeruhi ya mara kwa mara hivyo Moyes
anataka kikosi kitakachokuwa na nguvu ya kushindana na kuwania mataji makubwa
barani ulaya.
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako