Waumini wa Kiislam wakiuswalia Mwili wa Marehemu Jafari Ally Nje ya Nyumba yake, Bagamoyo jana Mchana |
Wakazi wa Bagamoyo wakibeba Mwili wa Marehemu Jafari Ally kwenda Makaburini |
Mume wa mwimbaji wa muziki wa taarabu hapa nchini, Khadija Kopa, ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Magomeni, Jafari Ally, amezikwa jana Majira ya saa Saba na nusu, katika makaburi yaliyopo mjini Bagamoyo
Msiba wa Ally umehidhuriwa na viongozi
mbalimbali akiwamo Waziri wa Elimu naMafunzo ya Ufundi, Shukuru Kawambwa, Mtoto
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ridhiwan Kikwete na viongozi
wengine mbalimbali wa CCM.
Akizungumza kwa machungu makubwa, Malkia
wa Mipasho Khadija Kopa, alisema amejisikia uchungu mume wake kufariki huku
akiwa nje ya jiji la Dar es Salaam, huku akirejea akimkuta mumewe ni marehemu.
Alisema kuwa msiba wa mumewe umempa
uchungu mkubwa, huku akiamini kuwa utaendelea kuwa kichwani mwake kwasababu ya
kuondokewa na mume wake aliyempenda.
“Nimeumia sana na msiba huu wa mume
wangu,” alisema Khadija Kopa, huku akibubujikwa na machozi.
Naye, Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani
Halmashauri ya Bagamoyo, Shukuru Mbato, alitumia muda mwingi kuwataka
Watanzania wakiwamo wakazi wa Bagamoyo kuishi kwa upendo sambamba na kumuombea
marehemu aishi kwa amani katika maisha yake mapya.
“Sisi tulimpenda sana, ila Mungu ndio
muweza wa yote, hivyo sisi kama binadamu lazima tukubali matokeo,” alisema
Mbato.
Marehemu Jafari Ally alifariki Dunia Juzi alfajiri katika
Hospital ya Lugalo Jijini Dar es Salaam kwa ugonjwa wa Kifua.
Inna Lilah wainalilah Rajiun
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako