Nelson Madiba Mandela
Raia wa Afrika kusini wamekesha kwa
maombi maombi nje ya makaazi ya zamani ya aliyekuwa rais wa taifa hilo Nelson
mtaani Soweto.
Rais Jacob Zuma amesema kuwa afya ya
shujaa huyo aliyepigana dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini humo inaendelea kuimarika.
Mandela aliye na umri wa miaka 94
amekuwa hospitalini akiuguwa ugonjwa wa maambukizi ya mapafu.
Awali mwanawe wa kike, Makaziwe
amesema afya ya babaake inaendelea kuwa njema.
Aidha Makaziwe amevikashifu vyombo
vya habari kwa kukita kambi nje ya hospitali alikolazwa shujaa huyo akisema
wanahabari wanapaswa kumheshimu babaake.
Rais Jacob Zuma alisema Alhamisi
kuwa hali ya Mandela iliimarika lakini bado yuko hali mahututi.
"leo angalau yuko sawa kidogo
kuliko nilivyomwacha jana usiku,'' alisema Rais Zuma baada ya kuongea na
madakatari wanaomtibu Mandela.
Bwana Zuma alifutilia mbali safari
yake ya Msumbiji ili kumtembelea Mandela hospitalini.
Wakati huohuo mwanawe Mandela
Makaziwe alisema Mzee 'bado yupo' na kuwa anaweza kuhisi mtu akimgusa.
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako