Thursday 6 June 2013

NGWEA aweka Historia mpya Mjini Morogoro



                  B O B pamoja na kina Mox, Venture na wadau wengine kaburini kwa Ngwea
                Gari iliyobeba jeneza ikiingia uwanjani Jamhuri, huku scout wakisindikiza.
             Jeneza limefika mahali pakuagia
                         Kaburi la Baba wa Albert Mangwea...R.I.P Faza Ngwea
   Mama Wa ALBERT Mangwea akitoka kuweka shada la maua kaburini kwa mwanae
 Mezz b akimsindikiza Mwanachemba mwenzake Uwanja wa Jamhuri MOROGORO
         Zola D alisimamia vizuri zoezi la kuaga mwili wa marehemu Albert Mangwea
          Tumpeleke msanii wetu kwenye makao yake ya Milele
   Afande Sele akiongea kwa niaba ya Wasanii wa Morogoro na kutoa shukrani zake za dhati kwa watu wote waliofika kuaga mwili wa Albert Mangwea
                                Godzilla pembeni yake kulia MADEE wakiingia Jamhuri stadium
                        Danny, Jide a.k.a anakonda,Rama d na Mansu lee
                       Madada zetu wakiwa nahuzuni moyoni kweli ilikuwa simanzi na majonzi...
                         Gelly wa RYMEZ, DJ Choka na Timbulo
                     Jay moe, P funk wakipata picha ya pamoja na wadau wa Morogoro




MSIBA wa Ngwea waweka historia mpya mkoani Morogoro kwa kuweza kufanyika kwenye uwanja wa Jamhuri na kuhudhuriwa na maelfu ya watu waliojikusanya kutoka mjini mpaka makaburini, kihonda kanisani ambapo ndipo mwili wa marehem Albert Mangwea umepumzishwa hapo.

Shughuli ya kuaga mwili wa marehem ulichukuwa takribani muda wa masaa matano kuweza kumalizika kwa hali ya utulivu uwanjani hapo. Watu walikuwa wengi hivyo kupelekea zoezi hilo kuendeshwa upesi ili kuupeleka mwili wa Mangwea katika nyumba yake ya milele.

Wasanii mbalimbali wamejitokeza kwa wingi kumuaga msanii mwenzao aliyekuwa akitamba kwenye tasnia ya muziki wa Hip hop nchini Tanzania na Afrika Mashariki.

Pata picha imekuletea matukio mbalimbali kupitia lenz yetu iliyonasa baadhi ya wasanii kwenye maeneo tofauti wakati wote wa kuaga mwili wa Albert Mangwea…Mungu Amlaze Mahali pema amiiin!!! 

Picha na Von Gasper, Dox Danta pamoja na Failasufa






No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako