Sunday 23 June 2013

STORI TATU ZINAZOHUSU KUONDOKA NA KUBAKI KWA ROONEY MAN CHESTER UNITED

Ronaldo na Rooney
1.Manchester united wamekiri kuwa Wayne Rooney hakuomba kuondoka na Alex Fergusson aliudanganya umma kwa kutoa taarifa kuwa Wayne Rooney ameomba kuuzwa na hivyo amewaomba Manchester united kumuomba radhi, Rooney ametanabaisha kuwa yuko tayari kubaki katika kikosi cha Mashetan wekundu hao wa jiji la Manchester united.
David Moyes kulia akisalimiana na Ferguson kati ya mechi zilizowahi kuwakutanisha Manchester united dhidi ya Everton
2.Magazeti ya ulaya yameripoti kuwa Mchezaji wa Manchester Unite Wayne Rooney atabadilishwa na Christian Ronaldo wa Real Madrid, habari hizo zimesema Madrid wapo tayari kumtoa Christian Ronaldo kwenda Manchester United na Man United wawape Wayne Rooney na Paund million 90.
3.Mchezaji wayne Rooney anatarajiwa kukutana na David Moyes kuzungumzia mustakabali wake na habar zimemnukuu mchezaji huyo akisema yupo tayari kuendelea kufungua kitabu kipya kwa kuendelea kubaki katika timu ya mashetai wekundu hao wa Manchester United.
Wayne Rooney akiwa na Moyes

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako