Sunday 30 June 2013

KAMBI YA KINA MBWANA SAMMATA YAKUMBWA NA BALAA GHANA

Kambi ya waliowahi kuwa mabingwa wa soka wa Afrika timu ya Tp Mazembe imekumbwa na balaa mara baada ya Nahodha wake Tresor Mputu kufiwa na mmoja wa kaka zake wakubwa aitwaye Ndombele maarufu kwa jina la Weah.
Wachezaji wa timu hiyo  akiwemo mtanzania Mbwana Sammata na Thomas Ulimwengu wapo Ghana kwa ajili ya mashindano ya ligi ya kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Hearts of Oak.walikusanyika zaidi ya saa moja katika chumba cha kiungo huyo kumfariji kabla ya uongozi haujapitisha uamuzi wa kumrudisha Congo kujumuika na ndugu zake katika msiba huo,.
Weah ambaye ni kaka wa mchezaji huyo alifariki tarehe 29 jumamosi hii mara baada ya kuugua kwa muda mrefu.
TRESOR MPUTU NAHODHA WA TP MAZEMBE

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako