Thursday 6 June 2013

Wakazi wa Morogoro wafurika kuupokea mwili wa Albert Mangwea

 Gari iliyobeba mwili wa marehem ikiingia nyumbani kwa Mama ALBERTY kihonda Mazimbu road
 P funk akiwasili eneo la tukio, hakika ni siku ya majonzi sana kwa wadau tasnia ya muziki wa kizazi kipya
                                 Kitale na wadau wengine
                           
                                   REST IN PEACE COWBAMMMMMMMA



Wakazi wa mji kasoro bahari, Morogoro jana walijitokeza kwa wingi kuupokea mwili wa Marehem Albert Mangwea ukitokea Dar es salaam mara ya baada ya Watu wa Dar es salaam kuuaga mwili huo na kuusafirisha mpaka mkoani Morogoro ambapo ndipo yupo Mama yake mzazi Albert Mangwea na Ndipo alipozikwa Baba wa Albert, Mzee Mangweha, na hatimaye ndugu yetu tutamzika hapo.

Wasanii wa Mkoani Morogoro walisogea mpaka mikese kwenda kuupokea mwili huo na kuweza kuusindikiza mpaka nyumbani kwa mama yake Mangwea aishie kihonda Mazimbu road.
Ratiba ya Mazishi itakuwa siku ya Alhamis mara ya Ndugu na jamaa kutoa heshma za mwisho kwa Mkali huyo wa freestyle Tanzania na Afrika Mashariki.

Ni watu wengi wamejitokeza kwenye msiba huu ambao kiukweli umegusa nyoyo za watu wengi sana kwa kuwa marehem alikuwa na kipaji cha pekee tofauti na wasanii wengine na hili limejidhihirisha kwenye kipindi cha uhai wake na mara alipofikwa na umauti
Sisi tulimpenda lakini Mungu amempenda zaidi, amsamehe na amlaze mahali pema…ameeen. 

Dox Danta

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako