Kikongwe, Jiroemon Kimura akisherehekea umri wa miaka 116
katika nyumba yake mjini Kyotango-Japan Photo: AFP/Getty Images
|
Jiroemon Kimura, amezaliwa mwaka 1897,
kafariki hospitalini mapema Jumatano na kifo chake kutangazwa na serikali ya
Japan.
Bwana Kimura, kutoka Kyotango - Kyoto
Prefecture, ndiye aliyekuwa akishikilia rekodi ya kuishi umri mrefu kuliko
binadamu wengine kwa mujibu wa Kitabu cha kumbukumbu duniani cha Guinness kilichotolewa
Desemba, 2012 na alifariki akiwa na umri wa miaka 115.
Mnamo tarehe 28 mwezi Desemba
alivunja rekodi ya Bwana Kimura kwa kutimiza umri wa miaka 115 na siku 253.
Hatahivyo, binadamu anayeshikilia rekodi ya kuishi umri mrefu kuliko wote
kutokana na rekodi zilizopo ni mwanamama wa Kifaransa, Jeanne Calment, aliyefariki
mwaka 1997 akiwa na umri wa miaka 122. (Lakini kuna Mtanzania Mzee Kitwala
alifariki mwaka 1992 akiwa na umri wa miaka 125, pia Mnepal Bir Narayan
Chaudhary, aliyefariki mwaka 1998 inasadikiwa alifarika akiwa na umri wa miaka
141, japo hawa wote hawatambuliwi na kitabu cha kumbukumbu GUINESS kwa kuwa
hawana vyeti vya kuzaliwa)
Bwana Kimura, alizaliwa mwaka 1897 Nchini
Marekani alisherehekea miaka 116 ya kuzaliwa mwezi wa nne (April) mwaka huu na
kupatiwa zawadi na Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe.
Wakati wa sherehe ya kumbukumbu ya
kutimiza miaka 116 Bwana Kimura alitembelewa na wazee zaidi ya 100 wenye umri
zaidi ya miaka 100 ili kumpa moyo wa kuishi miaka mingi zaidi.
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako