Sunday 9 June 2013

Washindi Wa KILI MUZIC AWARDZ


Kala Jeremiah na Izzo B




Msanii Wa Hip Hop NCHINI Kala Jeremia amewashukuru watanzania kwa kumuwezesha kunyakuwa Tunzo 3 za kili Music award usiku wa Jana pale Mlimani city
Tunzo hizi ni; Mtunzi Bora Wa mashairi ya Hip Hop
                        Wimbo bora wa Mwaka – Dear God
                        Msanii Bora wa Hip Hop
Tunzo zote amezipata kupitia wimbo wake wa Dear God uliopata umaarufu mkubwa sana hivyo kupelekea kuzoa tunzo tatu …Hongera sana Kala.

The Warriors
 

The Warriors From East wale wakali wa Reggae kama kawaida usiku wa jana walijinyakulia Tunzo yao ya Wimbo Bora wa Reggae( Song- Kilimanjaro)….Peace n Love kwao
 

Jide


Lady Jay DEE a.k.a Anakonda alidhihirisha ukali wake kwenye fani baada ya kubeba tunzo ya Msanii Bora Wa kike kwenye Tunzo za KILI Muzic awards


Recho apata tunzo ya Msanii Bora wa KIKE kwenye Bongo Fleva


 Ommy Dimpoz nae amejinyakulia Tunzo 3 ;Wimbo Bora wa Kolabo-ME & U ,Wimbo Bora wa POP na Video bora ya Mwaka

 
kulia Jay d akiwa na Rama dee


Wanaharakati wa Huu mziki RAMA DEE pamoja na Mapacha wametoa big up sana kwa watanzania kwa  kupeleka tunzo hiyo kwa wakongwe hao wa muziki ya Wakubwa Tanzania
Kupitia ukurasa wake wa Facebook K WA Mapacha aliwashukuru wadau na watanzania kwa ujumla kuweza kuwapigia kura za kutosha hatimae kudhihirisha ukali wao kwenye hili gem la Bongo
Tunzo kupitia wimbo KUWA NA SUBIRA –Rama Dee ft Mapacha……………………………………..
 









 Danta

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako