Saturday 15 June 2013

RAIA WAMPIGA BARAKA MASELE(BK) BAADA YA KUGONGA MTU, TANGA

Mchekeshaji Baraka Masele

Msanii wa Kundi la VITUKO SHOW Baraka Masele (BK) a.k.a Masele Cha Pombe amepata kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali baada ya kumgonga mtu barabara ya 14 mkoani Tanga leo Jioni. 

Polisi Wakiikagua Gari ya Baraka Masele baada ya ajali kutokea

 Habari za uhakika kutoka kwa mdau wa PATAPICHA zinasema kuwa Masele ni mzima japo kapata majeraha mwilini kutokana na kipigo hicho kutoka kwa raia.
Masele aligonga mtu ambaye hali yake bado mbaya hospitalini, baada ya tukio hilo Masele alisogeza gari mbele kidogo ili apaki, mara wananchi wenye hasira wakaanza kurushia mawe gari ya Masele (Toyota GDI) yenye namba za usajili T 940 AVD.

Kioo cha Gari ya Masele baada ya kuharibiwa na wananchi wenye hasira kwa mawe

Kufuatia hali hiyo Masele kwa kuokoa uhai wake aliamua kuwasha gari lake na kukimbia ambapo alijikuta akimgonga mtu mwingine japokuwa hakuumia sana, ndipo ilipomlazimu Masele kusimamisha gari na kuwapa nafasi raia wenye hasira kulivamia na kuliharibu vibaya kwa dhana mbalimbali za jadi, kwa kuvunja kioo cha mbele, taa za nyuma na tairi la nyuma kushoto, pia vioo vya pembeni (side mirror) vilivunjwa.

Tari la Gari ya Masele ikiwa imetobolewa na kitu chenye ncha kali

Usalama ulipatikana pale walipofika askari wa jeshi la polisi na kumchukua Masele hadi kituo cha Polisi Mabawa ambapo hadi PATAPICHA linatoka eneo la tukio bado Masele alikuwa amehifadhiwa kwa usalama wake.
Raia pia wameiba baadhi ya mali ikiwemo simu ya mkononi, hela na mali zingine ambazo thamani yake haijaweza kufahamika hadi sasa.

Uharibifu na wizi ndani ya gari ya Masele

Wasanii kadhaa wa maigizo na vichekesho wamefunga safari kwenda Tanga kuhakikisha habari zilizozagaa kupitia mitandao ya kijamii isiyofuata maadili ya uandishi wa habari iliyodiriki kuandika Baraka Masele amefariki. 

Baadhi ya wasanii waliofunga safari kwenda kuhakikisha habari za uzushi kuhusu kifo cha Masele, wakiwa wanatafakari pembeni mwa gari ya Masele

PATAPICHA inasikitishwa sana na Blog pamoja na Tovuti mbalimbali zilizoandika ya kuwa Baraka Masele amefariki Dunia.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako