Sunday 16 June 2013

BALLOTEL AFANYA VITUKO KABLA YA KOMBE LA MABARA BRAZIL.


Iko wazi kuwa endapo mtu atauliza swali kuwa ni mwanasoka gani duniani aliye na vimbwanga na vituko basi ni wazi kuwa kila mmoja atamtaja super Mario Balloteli kijana wa kiitaliano mwenye asili ya Ghana barani Afrika.
Ballotel akiwa na el shaarawy wakiiga sanamu ya yesu
Ni siku chache tu toka atoe maneno yenye utata kwamba endapo Real Madrid ingeshinda na kuitoa Borusia Dotmund kwenye michuano ya ulaya basi angemtoa mpenzi wake alale na kila mchezaji wa Real Madrid akiwemo Kocha wao kwa kipindi hicho Jose Mourinho.
 Ballotel akipiga picha za ukumbusho nchini Brazil
Kama kawaida yake akiwa  nchini brazil katika mji wa Rio de jenairo Super Mario na timu ya taifa ya Itala ikiwa matembezini kabla ya mchezo wao wa kukata utepe, Balotel anaonekana akipiga picha mbele ya sanamu ya yesu akiigiza sanamu hiyo maarufu inavyoonekana ndani ya mji huo wa Rio de jenairo nchin brazil na kuwafanya mashabiki wengi wakiacha shughuli zao na kuanza kumshangaa m,chhezaji huyo.
Ballotel na mchezaji mwenzake mbele ya dsanamu ya yesu nchin Brazil
Akiwa nchini Brazili mtukutu Mario alionekana akifuatwa na mashabiki wengi wakitaka kupiga nae picha za ukumbusho.
Ballotel na Stefan el shaarawy wakiangalia picha walizopiga nchini Brazil

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako