Sunday 16 June 2013

UCHAGUZI IRAN

Kiongozi wa chama chenye msimamo wa Kimhafidhina nchini Iran, Hassan Rouhani, ametangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais nchini Iran.
Hassan Rouhani akionyesha kidole chenye baada ya kupigia kura
Ikitangaza matokeo hayo Wizara ya mambo ya ndani nchini humo imesema, Bwana Hassan Rouhani ameshinda zaidi ya kura millioni kumi na nane, ambayo ni zaidi ya asilimia hamsini ya kura zote zilizopigwa.
Wizara hiyo imesema kuwa, idadi kubwa ya raia wa nchi hiyo walijitokeza kupiga kura kiwango ambacho kinakadiriwa kuwa asilimia sabini na tatu ya watu waliosajiliwa.
Meya wa mji wa Tehran, Mohamad Baqar Qalibaf, alimaliza katika nafasi ya pili katika kuwania kiti hicho cha urais

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako