Tuesday 25 June 2013

MANCHESTER UNITED KUMSAJILI CAVAN.

Picha ikimuonesha Cavan atakavyokuwa anaonekana akiwa na jezi ya Man united(si picha halisi)
Klabu ya Manchester united iko tayari kutoa ofa ya paundi millioni 50 kwa  Napol  kumsajili mshambuliaji Edison Cavan aweze kujiunga na Mashetani hao wekundu wa jiji la Manchester.
Rafiki wa nyavu Cavan akishangilia moja ya mabao aliyoifungia Napol
Habar zilizoandikwa na gazeti la Daily Mirror zinasema familia ya Glazzer inayomiliki timu ya Manchester United iko tayari kumpa David Moyes kitita cha paundi millioni 50 ili iweze kushinda vita ya baadhi ya klabu kubwa zinazomuwania mchezaji huyo zikiwemo Madrid na Manchester City.
Akiwa na uzi wa mazoez wa Napol
Moyes anatafuta mtu atakayekuwa pacha wa Robin Van Persie katika safu ya ushambuliaji na uchezaji wa nguvu na akili za kufunga mabao ndizo zilizomvutia David Moyes ingawa Napol wanaweza kukataa ofa hiyo kwani walishatangaza dau la mchezaji huyo ni paundi million 54
hivyo kama Manchester wanamtaka itabidi waongeze kitiota hicho.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako