Wednesday 19 June 2013

SOMA ALICHOKISEMA OKWI KUHUSU MCHEZO WAO WA KUFUZU KOMBE LA DUNIA DHIDI YA SENEGAL.



Mshambuliaji wa zamani wa simba anayekipiga na Etolie du sahel ya Tunisia Emanuel Anord Okwi ameamsha matumaini ya Uganda kufuzu hatua ya mtoano ya kombe la dunia itakayofanyika nchini Brazil mwakani kwa kusema watawafunga Senegal katika uwanja wao wa nyumban huko Dakar Senegal.
kikosi cha Uganda kabla ya kumenyana na Angola
Okwi alisema maneno hayo mara baada ya kumalizika kwa mtanange uliyowakutanisha wao(Uganda) na Angola  kaatika uwanja wa Nambole ambapo mabao yaliyofungwa na mshambuliaji huyo na Tom maweje yaliihakikishia Uganda kushika nafasi ya pili.
Muuaji wa Uganda Tom maweje  akimenyana na mchezaji wa Angola
Uganda inayoshika nafasi ya pili kwa kuzidiwa pointi moja na Senegal inayoongoza kundi hilo kwa kuwa na point tisa(9) ikifuatiwa na Uganda yenye point nane(8).
Emanuel Okwi akishangilia goli lake alilofunga dhidi ya Angola
Okwi alisema moyo wa upiganaji waliouonesha katika uwanja wa nambole kwa  kutoka wakiwa nyuma kwa goli moja kwa zaidi ya dakika 75 ndio utakaowawezesha  kuifunga Senegal katika ardhi ya nyumbani na kuwawezesha kufudhu kwa raundi ya mtoano.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako