Sunday 30 June 2013

UKWELI WA HABARI ZA THIAGO ALCANTARA KUJIUNGA NA MANCHESTER UNITED


KLABU ya Mashetani wekundu Manchester United imetuma ofa ya Paundi million 18 kuhakikisha inamsajili kliungo   Thiago Alcantara wa timu ya FC BARCELONA aweze kuitumikia timu hiyo msimu ujao wa mwaka 2013-2014.
Kama dili hillo litakamilika Thiago atakuwa anatia kibindoni mara tatu ya mshahara  aliokuwa akipokea katika timu ya Barcelona na atakuwa akipokea paund 140,000. Kwa wiki na  kumfanya  kuwa miongoni mwa wachezaji watakaokuwa wanalipwa pesa ndefu katika timu hiyo.
Chanzo cha kuaminika cha mchezaji huyo kilisema Thiago anajiandaa kuongea na viongiozi wa Barca juu ya ombi lake la kutaka kuondoka ndani ya kikosi hicho cha wakatalunya huku raisi wantimu hiyo akiwa na matumaini ya kumbakisha mchezaji huyo mara baada ya kuongea na mzazi wa Thiago aitwaye Mazinho.
Thiago aliwahi kusema huko mwanzo kutorizishwa na klabu hiyo haswa kutokana na kushindwa kujihakikishia nafasi ya kucheza game nyingi zaidi na hivyo kufanya samani yake kushuka kwa kiasi kikubwa.
Kama dili lake litakamilika Thiago atakuwa anapokea mshahara mkubwa zaidi ya Shinji kagawa,Dany welbeck, na Phil jones wanaolipwa paundi 810,000 kwa wiki.
THIAGO AKIWA NA JEZI YA TIMU YA VIJANA YA SPAIN ILIYOCHUKUWA UBINGWA WA ULAYA

THIAGO AKIWA NA JEZI YA MAN UNITED LAKINI SI PICHA HALISI

KUNGO HATARI THIAGO ALCANTARA AKIWA NA KOTI LA TIMU YAKE YA FC BARCELONA

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako