Saturday 29 June 2013

CHEICK TIOTE WA NEWCASTLE AKUBALI KUVAA JEZI ZENYE NEMBO YA KAMPUNI YA MICHEZO YA KAMARI CISSE AKIENDELEA KUWEKA NGUMU.

MCHEZAJI WA NEWCASTLE HATIM BEN ARFA AKIWA KATIKA POZI NA JEZI ZA WONGA
lile sakata linalowahusu wachezaji waumini wa dini ya kiislamu wa timu ya Newcastle kugoma kuvaa jezi za wazamini wapya wa timu hiyo zenye nembo ya neno WONGA limechukua sura mpya mara baada ya baadhi yao wakionekana kulegeza maamuzi yao na kuanza kukubali kufanya hivyo.
PAPIC DEMBA CISSE AKISHANGILIA MOJA YA MAGOLI ALIYOIFUNGIA NEWCASTLE AKIWA NA UZI WA MZAMINI WA ZAMANI
Habar zilizothibitishwa bna gazet la Daily Mirror la uingereza liomeripoti kuwa mchezaji Cheick Tiote ameshakubali kuvaa jezi yenye nembo hiyo na hivyo msimu ujao ataonekana akiwa ndani ya uzi wenye nembo ya wonga lakini tatizo lipo kwa Papis demba Cisse ambaye bado wanafanya nae mazungumzo.
Wonga bambayo ni kampuni inayohusika na michezo ya bahati nasibu maarufu kama kubet inaenda kinyume na sheria za dini ya kiislamu na wachezaji wa Newcastle Hatim Ben Arfa, Cheick Tiote na Papic Demba Cisse hawakuwa tayar kufanya hivo mchezaji ingawa Ben Arfa alishakubali na kufanya matangazo ya jezi hizo mpya.
MCHEZAJI CHEICK TIOTE MIONGONIO MWA WACHEZAJI WENYE ITIKADI YA KIISLAMU AKIFANYA VITU VYAKE NA TIMU YAKE YA NEWCASTLE

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako