Friday 14 June 2013

MOYES AFUFUA MATUMAINI YA KUMSAJILI RONALDO

Kocha wa timu ya Manchester United David Moyes ameamsha matumaini ya kumsajili Mchezaji wa zamani wa Manchester United anayekipiga  Real Madrid Christian Ronaldo mara  baada ya Mchezaji huyo kutoa taarifa za kukanusha  kutaka kusaini mkataba mpya na Klabu hiyo ya Real Madrid.

Ronaldo alitoa taarifa kupitia ukurasa wake wa tweeter kuwa habari zote zinazomuhusisha yeye na kutaka kusaini mkataba mpya na Real Madrid ni za uongo.
             Christiano Ronaldo wapili kulia                            

Moyes anataka kumrudisha Ronaldo katika timu yake ya zamani iliyompa umaarufu na mpango wa kupeleka ofa ya paundi millioni 60 tayari imeshatengwa ili kuweza kuwashawishi madrid kumuuza mchezaji huyo.

Wachambuzi wa masuala ya soka wanatoa nafasi kubwa kwa Ronaldo kurudi Manchester United haswa kwa kipindi hiki sababu Madrid watakapokataa kumuuza Ronaldo mpaka mkataba wake utakapoisha mwaka 2015 ataondoka bure bila ya wao kupata fungu lolote kutokana na mchezaji huyo atakuwa huru.

Raisi wa Real Madrid anataka kumbakisha Ronaldo mpaka mwaka 2018 muda wake wa uongozi utakapoishia ingawa kuna habari zikiihusisha familia ya kitajiri ya Qatar inayomiliki timu ya Monaco ya nchini ufaransa kuwa tayari kutoa paundi million 100 kumnunua RONALDO.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako