Friday 21 June 2013

PICHA ZA KIPIGO CHA MABAO 10-0, CHA SPAIN DHIDI YA TAHIT ZIPO HAPA

Tores akichezewa faulu na goliklipa wa Tahit iliyosababisha penati
Kama unadhani Fernando Tores ameisha na hana kiwango  basi utakuwa unajidanganya kwani mchezaji huyo ameibuka nyota wa mchezo baada ya kufunga magoli 4, katika ushindi wa magoli 10-0 dhidi ya Tahit.
El nino akishangilia moja ya mabao  yake katika mchezo huo
Tores alifunga magoli hayo 4 katika dakika ya 5, 33, 57,78, na kumfanya mchezaji huyo aondoke na mpira kama zawadi ya kufunga "hat trick" katika mchezo huo.
Wachezaji wa timu ya Taifa ya Spain wakimpongezaa Tores m ara baada ya kufunga bao kati,ka mchezo huo
Magoli mengine ya mchezo huo yaliwekwa kambani na kiungo wa timu ya Manchester City David Silva aliyefunga magoli 2 dakika ya 31, 89, na kumfanya atoke uwanjani akiwa ametumbukiza mpira nyavuni mara mbili.
 Katika mchezo huo uliokuwa wa uopande mmoja na uliokosa upinzani ulishuhudia mshambuliaji wa Barcelona David Villa akifunga magoli 3, "Hat trick na kuondoka na mpira wake,  magoli hayo aliyafunga katika  dakika ya 39,49,64.
Davi silva wa Spain akitumbukiza gozi la n'gombe kimiani na kuiandikia Spai bao.


Tores akiifungia bao la kuongoza timu ya spain katikla dakika ya 5 kipindi cha kwanza

Fernando Tores akishangila goli lake la 3, kwa ishara ya kuonesha vidole vitatu katika mchezo wao na Tahiti
Kiungo wa timu ya Chelsea alikuwa miongoni mwa wafungaji wa mchezo  huo kupitia bao lake alilolifunga dakika ya 66.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako