Mchezaji maarufu wa timu ya Manchester City Yaya
Toure, amewasili mjini Nairobi Kenya kwa uzinduzi wa muungano mpya wa
kukabiliana na uwindaji haramu kwa ushirikiano na shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia mazingira (UNEP).
Muungano
huo umeanzishwa ili kukabiliana na uwindaji haramu wa wanyama pori haswa Ndovu
ambao wanakabiliwa na tisho la kudidimia kutokana na uwindaji haramu barani
Afrika.
Toure,
mshindi wa tuzo la mchezaji soka bora zaidi Mwafrika kwa miaka miwili
mfululizo, 2011 na 2012 ataeleza kwanini amekubali kushirikiana na muungano huo
kupambana dhidi ya uwindaji haramu na nini hasa jukumu lake.
Anatarajiwa
kuongea na waandishi wa habari katika makao makuu ya Umoja wa mataifa katika
mtaa w akifahari wa Gigiri, Nairobi.
Wengine
watakaozungumza ni Achim Steiner mkurugenzi mkuu wa shirika la UNEP pampja na
mkurugenzi wa shirikisho la kandanda la kenya Sam Nyamwea.
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako