Tuesday 8 October 2013

KING MAJUTO KUWANIA KITI CHA UBUNGE TANGA



MCHEKESHAJI mkongwe nchini, Amri Athuman 'King Majuto' ametangaza nia yake ya kujitosa kwenye siasa akitaka kuwania Ubunge katika Jimbo la Tanga Mjini katika uchaguzi mkuu ujao wa 2015.

Akihojiwa na moja ya kituo cha radio jijini Dar es salaam, Mzee Majuto mwenye umri zaidi ya miaka 60, alisema Mungu akimjalia atajitosa kwenye ubunge jimboni humo kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), akidai kiu hiyo imechochewa na mafanikio ya wasanii waliojitosa kwenye siasa na kufanya vyema.
Mzee Majuto alisema, uzoefu alionao katika kuishi kwake mjini Tanga itamwezesha kuwatatulia kero na kuwaletea maendeleo ya kweli wananchi wenzake iwapo Mungu atamjalia katika kusudio lake.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako