Serikali Kikwazo
Wakati shinikizo la
Dunia sasa limeelekea kumaliza tatizo la ukwepaji kodi na Utoroshaji wa fedha
kutoka nchi za Kiafrika, serikali ya Tanzania inavuta miguu.
Moja ya njia ya
Serikali za nchi maskini kupata taarifa za makampuni makubwa ya kimataifa(MNCs)
yanayokwepa kodi ni mfumo wa kupashana taarifa (automatic exchange of tax
information) .
Kufutia shinikizo la
nchi mbalimbali, hivi sasa nchi zinazoitwa "secrecy jurisdictions"
(tax havens) Zimeanza kuweka sahihi makubaliano ya kutoa taarifa. Tanzania
mpaka sasa haijaweka sahihi na serikali haijatoa taarifa yeyote kwa Umma.
Ghana, Afrika Kusini
na Nigeria nchi zinazotegemea sana rasilimali kama Tanzania zimeweka saini
mkataba huu tayari. Asilimia 44 ya fedha za kigeni nchini zinatokana na mauzo
ya madini nje. Makampuni ya madini ndio yanaongoza kukwepa kodi.
Tanzania inapoteza
jumla ya dola za kimarekani kati ya milioni 500 na bilioni 1.25 kwa mwaka
kutokana na Makampuni makubwa ya kimataifa kukwepa kodi. Hii ni sawa na kusema
Tanzania inapoteza dola takribani milioni mbili kila siku kwa uporaji huu.
Naitaka serikali kutoa
taarifa kwa nini haichuki hatua kuzuia mwanya huu wa mapato ya Umma. Serikali
ichukue hatua mara moja kuhakikisha Tanzania inaingia makubaliano ya kupashana
taarifa za kikodi. Huu sio wakati wa kuvuta miguu katika suala nyeti la umma.
Badala ya kukimbilia kutoza kodi wanyonge, tuhakikishe makampuni makubwa
yanayonyonya rasilimali zetu yanalipa kodi inayotakiwa.
Zitto Kabwe, MB
Waziri Kivuli wa Fedha
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako