Wednesday 9 October 2013

IDADI YA MABILIONEA AFRIKA YAONGEZEKA

Imefahamika kwamba bara la Afrika lina mabilionea wengi sasa hivi kuliko ilivyokua ikifikiriwa ambapo hii imefahamika baada ya jarida la Ventures kuripoti kuwa pamoja na idadi ya mabilionea kuzidi kuongezeka bado asilimia kubwa ya Waafrika ni masikini wa kutupwa.
Kabla ya hii ripoti, idadi ya mabilionea wa Afrika ilikuwa 16 lakini imeongezeka na kufikia 55 na jarida hili limeweza kuwagundua mabilionea wengi kwa kuchunguza kwa siri ili kuepuka baadhi yao ambao ambao wanaficha taarifa za utajiri wao, yani huwa hawapendi  kuzitoa kwa wanahabari.
kati ya mabilionea hao 55, 20 wanatokea Nigeria na wanajumuisha wafanyabiashara wa mafuta huku Afrika kusini na Misri zikiwa na mabilionea tisa ambapo alietajwa kuwa ni tajiri kuliko wote Afrika ni Mnigeria Dangote ambae ana utajiri wa dola bilioni 20.2
Dangote alitengeneza utajiri wake kupitia biashara ya saruji na hadi leo anaongoza kampuni ambayo inahusika na biashara za unga wa kupikia, sukari pamoja na mafuta.
Mwanamke tajiri kuliko wote Afrika anatokea Nigeria pia ambaye Folorunsho Alakija ambae kampuni yake ya fama oil inamilki visima vya mafuta ambavyo alivipata mwaka 1993, alianza kama mwanafunzi wa masuala ya mitindo huko London na alikuwa akibuni mavazi ya rais wa zamani wa Nigeria Ibrahim Babangida.
Tajiri toka afrika kusini Nicky Oppenheimer ana utajiri wa dola bilioni 6.5 utajiri ambao ulipatikana kwenye madini hususan madini ya almasi ambayo amerithi toka kwa familia yake.
Pamoja na hii ripoti kunifikia bado haijanipa mabilionea wengine waliobaki wanatoka nchi gani… naendelea kufatilia

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako