Mtoto wa muigizaji mkongwe nchini,
Mzee Small, Wangamba Mahmud Said Wangamba ameiomba serikali na makampuni
aliyoyafanyia kazi baba yake kumsaidia gharama za matibabu ya baba yake
yaliyosimama kwa sasa kutokana familia hiyo kushindwa kumudu.
Akizungumza na mtandao wa filamucentral,
Mahmud alisema familia imeshindwa kuendeleza matibabu ya Mzee Small kwa muda
mrefu kutokana familia hiyo kuwa na kipato kidogo na kushindwa kumudu gharama
za matibabu na hivyo kuiomba serikali na makampuni aliyowahi kufanyanayo kazi
yaweze kumsaidia
“Sisi kama familia tunajisikia
vibaya sana tunaposhindwa kumsaidia baba kwa sababu yeye ni kila kitu, mimi
nasoma sina kipato, mzee toka mwaka jana mwezi wa tano mwaka jana alipomaliza
dawa zake hajatumia dawa hadi leo kwa sababu hatuna fedha,”
“Lakini jambo linalotuuma hakuna
hata kampuni ambayo imeonyesha kumsaidia kama Bakhresa alikuwa kuwa akifanya
nao kazi hakuna msaada lakini pia Serikali kupitia menejimenti utumishi wa umma
walikuwa wanafanya nao kazi wamemtosa yupo tu, pengine wanasubiri afe ndio waje
kumzika,”anasema Mahmud.
Mzee Small anasumbuliwa na ugonjwa
wa Kiharusi ikiwa sambamba na kupoteza kumbukumbu anahitajka zaidi ya milioni
moja na nusu kwa ajili ya matibabu kutokana na ushauri wa daktari kwani
inasemekana kichwani kuna tatizo ambalo linamsababishia kupoteza kumbukumbu
anahitaji dawa kwa ajili ya tatizo hilo na muda wa kupumzika.
Kwa
anayeguswa na tatizo hilo anaweza kuitumia familia yake mchango wa matibabu kwa
namba TIGO – PESA 0714 344 039 kumsaidia mzee Small.
SOURCE: Filamucentral
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako