Wednesday, 16 October 2013

MWANAMKE ALIYEMNYONYESHA NA KUMUAMBUKIZA MTOTO WA JIRANI AHUKUMIWA KUNYONGWA HADI KUFA

Mwanamke mmoja Mzimbabwe ambaye alimnyonyesha mtoto wa jirani yake bila kibali/ruhusa ya mama yake anakabiliwa na miaka miwili gerezani kwa kumwambukiza mtu mwingine HIV kwa kukusudia kwa sababu yeye ni mwathirika.
Mwanamke mwingine mwenye umri wa miaka 39 Annie Mpariwa alifika mahakama ya Gaborone Jumatano na kesi ilipangwa October 24 ili wafanye vipimo vya HIV kwa mara ya pili kwa mtoto huyo. 
Vipimo vya kwanza vilionyesha kuwa mtoto hajaathirika.
Mpariwa alikamatwa wiki iliyopita kwa kufanya kosa dogo kwa makusudi (ambalo ni kumnyonyesha mtoto bila kibali kutoka kwa mama yake) ila mtoto akipimwa kwa mara ya pili na kukutwa ni mwathirika adhabu itaongezwa na kuwa ya 'kumwambukiza mtu mwingine HIV makusudi'.
Mama wa mtoto huyo mwenye miezi 14 alisema kumuona jirani yake akimnyonyesha ilikuwa ni jambo la kushtusha sana kwake.
 
Aliendelea kusema kuwa jirani yake alimchukua mtoto wake aliyekuwa nje na kwenda kumficha chumbani kwake alikokuwa amepanga. Baada ya kumtafuta mtoto wake kwa muda mrefu,alienda kugonga hodi kwenye chumba cha Mpariwa lakini hakujibiwa.
Alipochungulia dirishani alimuona jirani yake huyo ambaye ni mwathirika wa ukimwi akimnyonyesha mtoto wake.
"Nilipochungulia dirishani nilimuona akimnyonyesha mtoto wangu.Nilipata mshituko mkubwa karibu nizimie",aliongezea kusema kwamba maziwa ya jirani huyo yalikuwa bado yanavuja na inashangaza kwasababu kwa muda huo yeye hakuwa na mtoto ambaye anamnyonyesha(hakuwa mzazi) wala hakuwa mjamzito.
Tukio hilo limekuja kwenye mwamko wa sheria mpya zilizowekwa kuhusu HIV na AIDS ambazo zimekuja na adhabu kali kwa wale wanaowaambukiza wenzao virusi vya ukimwi makusudi.
Ila jamani kuna watu wakatili kweli duniani,sasa jirani alikuwa anataka amwambukize ili iweje? Au anapata faida gani? Such an innocent child,kafanya nini to deserve such a bad,horrifying and unbearable thing on her life(HIV)? Kwanini watu hawana huruma siku hizi?!! Inasikitisha sana.....

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako