Tuesday, 29 October 2013

TAMASHA KUBWA LA AMANI NA UPENDO LASHIKA KASI

 
Lile tamasha kubwa la injili linalokwenda kwa jina la "TAMASHA LA AMANI NA UPENDO" linazidi kupamba moto kwenye upande wa maandalizi ambapo waimbaji wa Nyimbo za Injili wanaendelea kuongezeka kila siku zinavyozidi kwenda mbele ambapo hadi kufikia leo wa waimbaji wa Nyimbo za Injili na kwaya wameongezeka na kufikia zaidi ya 50 akiwemo, Rose Mhando, Bahati Bukuku, Boni Mwaitege, Neema Gasper, Madam Ruti, Upendo Nkone, Edson Mwasabita,  Happy Kamili, Martha Baraka,  Frola Mbasha, Siza Mwampamba, Prisca Mwalugaja, Elizabeth Nzunda, Davdi Robert, Adelina Swai, Jackline Falles, Sara Mvungi, Victor Aron, Danny Bandezu, Kwaya za Dar es Salaam Gospel na AIC Vijana Chang'ombe Choir (CVC) na waimbaji chipukizi wa Nyimbo za injili kibaaaaaaaaaaao.
Mpenzi wa Muziki wa Injili kaa Tayari tumwabudu Mungu kwa Nyimbo za Injili huku tukiombea amani Taifa letu la Tanzania, Tarehe, 8  Desemba, 2013 siku ya Jumapili ambayo kesho yake Jumatatu itakuwa ni Sikukuu ya Uhuru wa Tanganyika (Hivyo itakuwa ni siku ya mapumziko ya kitaifa)
Kwa kiingilio kidogo kabisa kisichotegemewa na wengi ili tuweze kumudu asilimia kubwa ya watanzania na wapenzi wote wa nyimbo za injili tuweze kuhudhuria. (Tsh 5,000/= kwa mtu mzima na Tshs 2,000/= kwa watoto) Utakosajeeee.
Tamasha litafanyika Jumapili (8-12-2013) katika viwanja vya ustawi wa Jamii kuanzia saa 5 asubuhi hadi saa 12 Jioni.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako