Wakazi wa jiji
la Dar Es Salaam wamejitokeza kuaga mwili wa mama mzazi wa mwandishi wa ITV
Radio one Ufoo Saro marehemu Anastazia Saro katika kanisa la kiinjili la
kilutheri Kibwegere Kibamba kabla ya kusafirishwa kwenda Moshi kwa mazishi.
Kutokana na msiba huo,ITV ilianza kwa kufika katika hospitali ya taifa
ya Muhimbili ili kumjulia hali mwandishi wa ITV Ufoo Saro aliyelazwa katika
hospitali hiyo ambapo afisa uhusiano wa hospitali hiyo bwana Aminiel Aligaesha
amesema anaendelea vizuri.
Baada ya afya ya Ufoo Saro inavyoendelea, ITV ilitia kambi katika chumba
cha kuhifadhi maiti katika hospitali hiyo na kushuhudia mwili wa Anastazia Saro
ukiondolewa na kupelekwa Kibamba nyumbani kwake ambapo umati mkubwa wa watu
walipokea mwili huo kisha kuingizwa ndani huku vilio vikitawala.
Mwili
ulifikishwa katika kanisa la KKKT Kibwegere Kibamba na kupokelewa na umati
mkubwa wa watu waliofika ndani ya kanisa hilo,ambapo mchungaji wa kanisa hilo
Magreth Chikolowa amesema kuwa kuna vifo vingine vinatokea lakini si kwa kusudi
la Mungu huku msemaji wa familia akieleza historia fupi ya marehemu.
Mkurugenzi wa
ITV Radio one Bi Joyce Mhaville kwa niaba ya mwenyekiti wa makampuni ya IPP Dr
Reginald Mengi amesema wamepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mama yake Ufoo
na kwamba mbali na kuwepo hapo kwa ajili ya mwenyekiti wa makampuni ya IPP
lakini ameagizwa na Ufoo Saro kumwakilisha katika kumuaga mama yake huku
mwenyekiti wa kamati nzima wa msiba huo akitoa shukrani kwa mwenyekiti wa
makampuni ya IPP kwa kufanikisha safari ya kusafirisha mwili huo kama
anavyoeleza.
Ndugu jamaa na marafiki waliaga mwili huo kwa
majonzi huku baadhi ya wafiwa wengine wakishindwa na kupewa msaada wa kushikwa
huku vilio vikitawala ambapo marehemu Anastazia Saro ameacha mtoto mmoja Ufoo
Saro na mjukuu mmoja Alvin ambapo anatarajia kuzikwa katika kijiji cha Shali
Machame mkoani Kilimanjaro
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako