Saturday 26 October 2013

NEY WA MITEAGO NUSURA AKUTANE NA KISAGO CHA POLISI KWENYE SHOOTING

 


Rapper Ney Wa Mitego amesema kuwa hii picha hapo juu ni tukio wakati wana shoot video ya wimbo wake Unaofanya vizuri kwa sasa kwenye radio stations ' Salam Zao', na ndipo wakatokea watu waliodai kuwa ni askari.

Ney Wa Mitego Amesema ' Nikweli nilituwa sero jana baada ya raia wasio julikana kuleta fujo eneo la kazi yangu  kwa sababu kulikuwa na waigizaji waliokuwa na sare za polisi. Watu hao
sijuani nao na walijitambulisha kama askari na kutaka kujua kwanini natumia sare za polisi kwenye video yangu bila kibali. hicho ndio kitu kilichopelekea nikapelekwa polisi.

Mitego ameendelea kusema kuwa baada ya kukaa sero kwa dakika kama 15 mkuu wa kituo alikuja na kusikiliza tatizo hilo na ndio aliachiwa huru baada ya kutoa maelezo kuhusu tukio hilo na sare hizo kuoneknaA uraiani.

Ney aliwekwa sero Kwenye kituo cha polisi Urafiki kilichopo Manzese na wiki ijayo video hii itaonekana kwenye vituo vya television Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako