Friday 11 October 2013

MWANANCHI AWA HURU KUMWAGA HABARI KWA RAIA BAADA YA KIFUNGO CHA SIKU 14

MKURUGENZI MTENDAJI WA MWANANCHI COMMUNUICATION BWANA TIDO MHANDO


Kupitia mtandao wake MWANANCHI imeandika taarifa ya kutoka kifungoni, na jinsi ambavyo adhabu hiyo ilivyowapa hamasa kubwa imewaathiri watu mbalimbali wakiwemo waandishi, vijana wanaosambaza na wengine, pia wameeleza msimamo wao baada ya adhabu hiyo. PATA PICHA inakupata stori kamili
“Hatua ya kulifungia gazeti hili kwa sababu za kufikirika imesababisha maumivu kwa watu wengi. Vijana (vendors) waliokuwa wakiuza na kusambaza gazeti hili pamoja na familia zinazowategemea wameumia. Waandishi wa kujitegemea wanaolipwa kutokana na habari wanazotuma gazetini wameumia pamoja na familia zao.
Tumetoka kifungoni tukiwa na somo muhimu. Kwamba sheria kandamizi kama Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 haisimamii masilahi ya taifa, bali kundi la watu wachache. Ni sheria kandamizi ambayo kwa umoja wetu tunaweza kuifuta. Tungependa kuwashukuru wasomaji wetu na wananchi kwa jumla kwa kuwa nasi katika kipindi kigumu tulichokuwa kifungoni. Vilevile, tunavishukuru kwa namna ya pekee vyombo vyote vya habari vya ndani na nje ambavyo vilisimama imara kupinga hatua ya Serikali kufungia magazeti.
Tutakuwa watu wasio na shukurani kama hatutatambua mshikamano mkubwa ulioonyeshwa na asasi za kiraia, mabalozi na watu mbalimbali kupinga matumizi ya sheria hii kandamizi. Hatujakata tamaa, bali tumetoka kifungoni tukiwa na hamasa kubwa kuendelea kuwapa habari wananchi pasipo woga wala upendeleo.
Hatupambani na Serikali, lakini tutaendelea kuikosoa pale inapofanya makosa na tutaipongeza pale inapotimiza wajibu wake. Tunawaomba wasomaji wetu mwendelee kutuunga mkono”.
SOURCE: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako