Tuesday 15 October 2013

BABASTYLES AVUNJA UKIMYA KUHUSU YEYE NA MUZIKI


Gwiji la Muziki wa Bongoflava mwenye nyimbo za vituko Noorah Haji a.k.a BabaStyle amevunja ukimya kwa kuamua Kufunguka kile kilicho moyoni mwake kuhusu ukimya wake kwenye Game kwa sasa ambapo amefika mbali na kusema kuwa Muziki hauna faida kwake na kwa sasa anaufanya Muziki kama Starehe like mtu anavyotoka kwenda Bar kunywa beer huku akiwa sio Mlevi means siku akifeel hamu tu.
Noorah ameelezea ukimya wake ambao yuko nao kwamba Kwa sasa muziki hautegemei tena kwamba utakuja kumpa faida kwani ameusotea kwa muda Mrefu sana bila Mafanikio na kusema kuwa Hana time nao tena bali ana mambo mengi ya kufanya yanayomuendeshea Maisha yake na sio muziki ila ataufanya tu kama sehemu ya Starehe.
Amejaribu kufafanua kuhusu wingi wa Wasanii kuwa wengi Nchini huku wenye Mafanikio wakiwa wachache ambao pia amewataja kama watu wa kusifiwa wana hela ila sio kiivyo ambapo wanasemwa wamefanikiwa kumbe ni maneno tu (Politics kwenye muziki).

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako