Tuesday 29 October 2013

MMWANAUME MREFU KULIKO WOTE DUNIANI AFUNGA PINGU ZA MAISHA


 
Mtu anayeshikilia rekodi ya kuwa na urefu kupita wote duniani Bwana Sultan Kosen mwenye futi 8.3 amefunga ndoa majuzi na mwanamke wa ki-Syria anayemwita “mpenzi wa maisha yake”
“siwezi kuelezea kwa maneno jinsi ninavyojisikia” alisema Kijana huyo mwenye umri wa miaka 31 katika sherehe za Harusi zilizofayika kusini kwa mji wa Mardin Jumapili iliyopita

“Nina furaha kupita kifani ndani ya dunia hii”alinukuliwa akielezea katika moja ya tovuti zinazotoa habari kuhusu watu wanaoshikilia rekodi za dunia.

Mke wake Sultan, ajulikanaye kwa jina la Mervi Dibo, mwenye uri wa miaka 20 kutoka Syria alisema “nina imani hii furaha itadumu milele daima katika maisha yetu”

Mtu Mrefu alivalia suti Nyeusi iliyohitaji Kitambaa cha Mita 6 ili itoshe vazi zima la suti yake.

Sultan amezaliwa katika familia ya wakulima kusini mwa Uturuki, na mwaka 2009 alishinda rekodi ya Guiness ya Dunia kama mwanaume mrefu kuliko wanaume wote Duniani akiwa na urefu wa Meter 2.47.

Urefu wake ni matokeo ya Homoni alizonazo mwilini, kutokana na maelezo ya Madaktari wa Virgina waliokuwa wakimfanyia uchunguzi.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako