Katika hali ya kusikitisha na ya ukali wa hali ya juu dereva bodaboda aliyefahamika kwa jina moja la Mbikano anasakwa na jeshi la polisi Mkoani Mtwara kwa kusababisha mauaji ya mtoto mdogo ambae alimgonga wakati akiendesha bodaboda yake na kumuumiza mguu kisha akambeba na kukimbia nae na baadae kumtupa kwenye kichaka na fisi wakaja kumla na kubakisha fuvu
Habari za uhakika zilizonaswa na mwandishi wa Xdeejayz aliyeko Masasi na Mtwara zilisema tukio hilo la kusikitisha limewaliza watu wengi, akiongea na xdeejayz kwenye mahojiano maalum mjomba wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina la Mjomba wa mrehemu Yusuph Hashim (30) alisema tukio hilo lilitokea tarehe 29 Septemba, 2013 majira ya saa 12:30 jioni.
Mjomba huyo aliendelea kueleza kuwa siku hiyo mtoto huyo aliyeitwa kwa jina la Shabiru Muhidin (4) ambapo wanaishi katika Kijiji Mkaseka wote na mtoto huyo muda huo alikuwa ametumwa dukani na mama yake mzazi aliyefahamika kwa jina la Thawabu Hakhim Nakanje.
Hata
hivyo katika ha ilisiyotajia mjomba huyo alisema kuna kundi la vijana waliokuwa
wanatoka kwenye kutizama mpira kwenye kijiji cha Jirani cha Mkururu huku
wakiwa wamepakizana kwenye bodaboda walivyofika maeneo ya Mkaseka ndipo
walipomgonga mtoto huyo na kumjeruhi mguuni na walipoona watu wameanza kujaa
ndipo walipomchukua mtoto huyo ambae alikuwa akilia kwa uchungu na kuondoka nae
kusikojulikana.
Mjomba
huyo aliendelea kuileza xdeejayz kuwa kijana huyo aliyekuwa anaendesha bodaboda
aliendelea kutokomea kizani na mtoto huyo hadi alipofika mahali penye msitu mkubwa
alimrusha kichakani huku mtoto huyo alimsihi asimuache msituni hapo kwani
angeliwa na wanyama lakini bila huruma dereva huyo wala hakujali hatimaye
alimuacha mtoto huyo.
Habari
zaidi ziliendelea kusema huku nyuma alipogongewa mtoto habari zilianza kusambaa
ambapo mjomba huyo alipopata taarifa hizo aliondoka na majirani zake kuelekea
kwenye zahanati ya kijiji hicho kwa kudhani huenda watu hao waliamua kufanya
ubinadamu kwa kumpelekea hospitali baada ya kumuumiza ambapo alipofika kwenye
zahanati hiyo hakumkuta mtoto huyo.
Baada
ya kumkosa kwenye zahanati hiyo walienda kwenye kituo kikubwa cha Afya cha Nagaga
lakini hapo napo hawamkuta ndipo walishauriana kwenda kuripoti kwa mkuu wa
polisi jamii na mara baada ya kukutana na kamanda wa polisi jamii aliyefahamika
kwa jina la Hamis na baada ya kuwasikiliza aliitisha kikao cha dharula na
wakaanza kumtafuta mtoto huyo hapo ilishakuwa siku iliyofuata ambapo baada ya
msako kufanyika walienda hadi kwenye sehemu moja yenye kilima msitu.
Baada
ya kufika kwenye mlima huo waliona mburuzo ulioambatana na damu na walipoenda
mbele zaidi waliona damu nyingi zikiwa na vimetapakaa na vipande vya utumbo na
fuvu kipande kidogo tu hali waliyogundua kuwa mtoto huyo alishapoteza uhai wake
kwa kuliwa na fisi ambao eneo hilo wako wengi kama mbuzi.
Kufuatia
kushuhudia hayo kamanda wa ulinzi shirikishi alipiga simu kituo cha polisi
Masasi ambapo polisi walifika haraka na kupiga picha eneo la tukio huku
wakiondoka na mabaki ya fuvu hilo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Hata
hivyo hadi sasa mmiliki wa bodaboda hiyo anashikiriwa na jeshi la polisi huku
mtuhumiwa namba moja akitafutwa kwa udi na uvumba ili kufikishwa mbele ya mkono
wa dola.
Xdeejayz ilifanya jitihada za kumtafuta
kamanda wa polisi Mkoa wa Mtwara ili kuzungumzia ambapo baada ya kupigiwa
simu ilipokelewa na mlinzi wake huku akisema kuwa Kamanda yuko bize na vikao
hivyo atafutwe jioni ya leo.
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako