HATUA ya Mbunge wa
Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe kutaja hadharani mshahara wa Rais na Waziri Mkuu,
imechukua sura mpya baada ya Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya
(TUGHE) kulaani hatua hiyo na kuomba Spika Anne Makinda kuchukua hatua kwa vile
ni ukiukaji wa sheria.
Chama hicho kimeeleza kusikitishwa na kitendo hicho kufanywa na Mbunge aliyehusika na upitishaji wa sheria hiyo huku wabunge wenyewe wakiwa wakali pale wananchi na wadau mbalimbali wanapohoji mapato yao.
Chama hicho kimeeleza kusikitishwa na kitendo hicho kufanywa na Mbunge aliyehusika na upitishaji wa sheria hiyo huku wabunge wenyewe wakiwa wakali pale wananchi na wadau mbalimbali wanapohoji mapato yao.
Alisema ajenda ya wafanyakazi kwa sasa ni kuona wabunge wanapigana kufa kupona katika kuhakikisha kuwa mshahara wa mfanyakazi unaongezeka kukidhi mahitaji ya mwezi mzima na kuwaondolea mzigo wa mikopo inayowaandama.
Alisema pamoja na hilo ni mkakati wa wafanyakazi sasa kuona wabunge wanatumia muda wao uliosalia kabla ya Bunge kuvunjwa kuhakikisha mambo makubwa mawili yanaingizwa katika Katiba mpya, moja ikiwa ni nafasi ya mfanyakazi kikatiba ikoje na pia kuona Katiba mpya inasema nini juu ya hatima ya maslahi ya wafanyakazi.
“Tunataka Katiba mpya itamke wazi juu ya mishahara ya wafanyakazi ili iwe ni ile inayokidhi haja,” alisema.
Aeleza kuwa ni jambo la kusikitisha kuona wabunge wanaanza kutaja mishahara ya viongozi wa taifa hadharani kwa kudhani kuwa ndio njia sahihi ya kuwasaidia Watanzania bila kujua kuwa hatua hiyo itasababisha mgawanyiko wa matabaka na kuligawa Taifa, jambo ambalo ni la hatari.
“Sisi mishahara ya viongozi wote tunaifahamu na hata ya wabunge, lakini sheria
inasemaje juu ya kutangaza mshahara wa mtu hadharani? Wafanyakazi wanaweza
kuitaja lakini kwa vile wameandaliwa hawafanyi hivyo, wanazingatia sheria,
kanuni na taratibu za nchi.
“Naamini kama wafanyakazi wangekuwa ni watu wa kukusanyana na wangekuwa hawana maadili wangeweza kusema mengi ambayo yangeshangaza jamii lakini hawafanyi mambo kwa kukurupuka au kuutafuta umaarufu usio na msingi,” alisema.
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako