Sunday 27 October 2013

BALOZI ISAAC ABRAHAM SEPETU (BABA YAKE WEMA) AFARIKI DUNIA ASUBUHI YA LEO


 
Taarifa  tulizozipata  asubuhi hii zinaarifu  kuwa Balozi Isaac Abraham Sepetu   ambaye  ni  baba  mzazi  wa  Miss Tanzania (2006) Wema  Sepetu ameaga dunia, leo asubuhi kwenye Hospital ya TMJ Mikocheni Jijini, Dar es Salaam
Balozi Sepetu alikuwa amelazwa kwa miezi kadhaa kutokana na  maradhi ya kiharusi na kisukari  na  mipango ya mazishi inafanyikia nyumbani kwa marehemu maeneo ya Sinza-Mori jijini Dar.
Balozi Sepetu aliwahi kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje mnamo miaka ya 1970 wakati wa utawala wa awamu ya kwanza chini ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.  
Vilevile, aliwahi kuwa balozi nchini Urusi tangu mwaka 1982 wakati wa utawala huohuo wa Nyerere. Machi 27, mwaka huu, Balozi Sepetu aliteuliwa na Rais wa Zanzibar, Dk Mohammed Shein,  kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitega uchumi ya Zanzibar (ZIPA), Hadi mauti yalipomkuta

Blog hii ya PATAPICHA inaungana na waombolezaji wote wa Msiba huu na Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma na Mwenye Kurehemu, Aiweke mahala pema peponi roho ya Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu 

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako