Monday 14 October 2013

MWANDISHI WA HABARI WA ITV/RADIO ONE APIGWA RISASI NA KUJERUHIWA VIBAYA, MAMA YAKE AUAWA


Mtu mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Bwana Anthery Mushi, amempiga risasi Mwandishi wa Habari wa ITV/Radio One , Ufoo Saro na kumjeruhi vibaya.
Aidha Anthery Mushi amempiga risasi  kumuua mama yake mzazi  Ufoo Saro na kisha kujiua, katika tukio lililotokea leo asubuhi maeneo ya Kibamba CCM, Wilayani Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
Ufoo Saro Mara baada ya Kufanyiwa Upasuaji wa kutolewa Risasi mwilini

Kamanda wa Polisi wa Kanda ya Kinondoni, Bwana  Camilius Wambura  amesema tukio hilo limetokea saa 12 na nusu leo asubuhi na kusema inadaiwa kuwa Anthery Mushi ni mume au mchumba wa Ufoo Saro  anafanya kazi Umoja wa Mataifa na kituo chake cha kazi ni nchini Sudan.
Ufoo Saro akirudishwa wodini baada ya kufanyiwa Upasuaji kutolewa risasi mwilini

Kamanda Wambura amesema Anthery Mushi  alirejea jana kutoka Sudan na leo majira ya saa 12 waliondoka yeye  na Ufoo Saro  wakitokea eneo la Magari Saba kwenda kwa Mamake  Ufoo Saro, Kibamba CCM.
Waandishi wa Habari wakipiga picha Mwandishi Ufoo Saro baada ya Kutolewa chumba cha upasuaji

Amesema kilichoendelea huko bado askari wanaendelea na uchunguzi, lakini taarifa zinasema walipofika huko Anthery Mushi alichukua bastola na kumpiga risasi  kifuani mama mzazi wa Ufoo Saro na  na kisha kumpiga Ufoo risasi  tumboni na mguuni  kisha yeye kujipiga risasi juu ya kidevu na kufariki dunia papo hapo.
Waandishi wa Habari wakimsindikiza Mwandishi Ufoo Saro baada ya Kutolewa chumba cha upasuaji

Ufoo Saro alikimbizwa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako anapatiwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri.
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dakta Reginald Mengi, amefika katika hosptiali hiyo kumjuilia hali  Ufoo Saro

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako