Mrwanda
anasema: “Kama mchezaji, nimejifunza kutokana na mazingira kupitia maisha
wanayoishi wachezaji wengine waliotutangulia, nikakuna kichwa,
nikajipanga.”
MAISHA
yanahitaji kitu gani tena? Ukiwa na akili na ukiitumia vizuri akili yako,
utapiga bao la maisha. Hiki ndicho alichokifanya straika Mtanzania, Danny David
Mrwanda. Ndio maana marafiki zake huwa wanamtania kwa kusema kuna ‘Mrwanda
mmoja tu duniani.’
Si kosa
kusema, Mrwanda ni milionea, kutokana na utajiri
alionao anaweza kuishi maisha yoyote anayotaka bila hata kucheza soka. Kazi
yake ni soka, fedha anazopata kutokana na soka kama usajili, mshahara na posho
aliwekeza na sasa ukimtaja Mrwanda unamzungumzia mwanasoka mwenye mali za
maana.
Anaweza
kuingiza zaidi ya Sh350,000 za Kitanzania kwa siku sawa na Sh15 milioni kwa
mwezi, kupitia vitega uchumi vyake vya biashara anazomiliki Tanzania.
Mrwanda
alishtuka mapema na kupanga mambo yake, alitunza pesa na kufanya mambo ya
maendeleo akiogopa kuumbuka baada ya kustaafu soka kama inavyotokea kwa wachezaji
wengi.
Mrwanda
anasema: “Kama mchezaji, nimejifunza kutokana na mazingira kupitia maisha
wanayoishi wachezaji wengine waliotutangulia, nikakuna kichwa, nikajipanga.”
Utajiri wake
Maisha
anayoishi Mrwanda jijini Dar es Salaam anastahili kuitwa staa na profesheno wa
ukweli. Anamiliki nyumba kubwa ya kisasa iliyopo Kisukuru, Tabata, Dar es
Salaam. Kwa haraka makadirio ya thamani ya mjengo huo ni Sh 200 milioni.
Anamiliki
usafiri wa nguvu aina ya Nissan Murano, gharama yake ni kama Sh60
milioni. Mbali na hivyo, anavyo viwanja vinne vyote viko jijini Dar es
Salaam kati ya hivyo viwili ameshaanza kujenga na shamba la ekari moja lililopo
King’azi, Kinyerezi, Dar s Salaam.
“Mpango wangu
ni kujenga nyumba za biashara kama hapa (anaonyesha kiwanja kimoja ambacho kipo
karibu na nyumba anayoishi hapo Kisukuru), unaona nimeanza kujenga fremu za
duka kwanza huku, kule kwingine naangalia kwanza, naweza kujenga nyumba ya
kulala wageni au kupangisha.
“Lile shamba
kule bado nalima mazao mbalimbali na kufuga tu, ila nina mpango mkubwa hapo
baadaye kwa sasa naangalia kwanza upepo ili nifahamu niweke kitu gani
kitakachoniingizia kipato,” anasema Mrwanda.
Mbali na
ardhi, ukikutana na daladala yoyote kwa nyuma imeandikwa ‘Mrwanda The
Straika’ kwa chini ‘Maximo’ na mbele ‘Royal Prince’ usijiulize mara mbili
kutaka kujua ni za nani? Ni mali ya Mrwanda.
Mrwanda ndiye mmiliki wa daladala hizo, anazo nne,
mbili zinafanya safari za Mwenge-Kariakoo na nyingine Mwenge-Posta. Kila
daladala moja, inapeleka hesabu ya Sh85,000 kwa siku, ukizidisha mara nne idadi
ya daladala hizo ni Sh340,000 kwa siku.
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako