Tuesday 8 October 2013

MADAM RITA AOMBA KURA ZA WATAZAMAJI EPIQBSS



Shindano la kuimba la Epiq BSS limeingia hatua za mwisho wiki hii likiwa limebakiza washiriki kumi na mbili, kuelekea kumpata mshindi wa shilingi milioni hamsini pamoja na mkataba wa kurekodi.
Washiriki waliochaguliwa kwa usaili wa simu, nao waliungana na wenzao walioingia kumi bora wiki hii na konyesha uwezo mkubwa, hali inayoashiria kutakuwa na kazi kubwa kumchagua mshindi.
Washiriki waliobaki mpaka sasa na namba zao za ushiriki ni Amina Chibaba (03), Elizabeth Mwakijambile (08), Emmanuel Msuya (21),
First Godfrey (11), Francis Flavian (09), Furaha Charles (14),
Furaha Mkwama (06), Joshua Kahoza (02), Maina Thadei (5), 
Mandela Nicholas (10), Melisa John (22) na Raymond John (23).
Akizungumzia hatua ambayo shindano limefikia, jaji mkuu wa shidano hilo, Ritha Paulsen, aliwataka wananchi watumie vema nafasi ya kupiga kura kwa kuchagua washiriki wenye vipaji vikubwa.
‘Hatua hii ni muhimu sana, hasa kwa kuwa inalirudisha shindano kwa wananchi ili waweze kumchagua mshindi wao, hivyo nawaomba wawapigie kura kwa wingi’ alisema Ritha.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako