Picha za wanajeshi wa Kenya waliokwenda katika
jumba la Westgate katika juhudi za uokozi na kisha baadaye kuonekena kwenye
kamera za CCTV wakiondoka na mifuko ya plasitiki yenye bidhaa za madukani, bila
shaka zimewashangaza wengi. Picha hizo mwanzo zimeonyesha wanajeshi
wakiingia ndani ya jengo hilo wakiwa wamebeba silaha kukabiliana na wanamgambo
walioshambulia jengo hilo wiki nne zilizopita na baadaye wakitoka wakiwa
wamebeba mifuko hiyo wakiwa na silaha zao kwa wakati mmoja.
Pamoja na picha za wanajeshi wakiwa wamebeba
mifuko, pia kulikuwa na picha zengine zilizoonyesha mashine ya pesa zikiwa
zimeporwa ndani ya migahawa huku picha za alama za risasi kwenye maeneo ya
kuhifadhia pesa, pia zikionekana.
Inaarifiwa ilikuwa jaribio ya kufungua hifadhi
hizo ambalo halikufanikiwa.
Madai haya ya wanajeshi kufanya uporaji wa
maduka katika jengo hilo, yalikanushwa vikali na jeshi la Kenya kiasi cha
kutaka hatua kuchukuliwa dhidi ya waliokuwa wanatoa madai hayo, lakini
haijulikani jibu lao litakuwa nini hasa kwa picha hizo za CCTV zilizoonyesha
wanajeshi hao wakifanya uporaji.
Wamiliki wa maduka waliorejea kwenye maduka
yao baada ya shambulizi, walidai kuwa maduka yao yaliporwa ingawa jeshi
lilikanusha madai hayo baadhi ya taarifa zikisema kuwa ilikuwa njama ya wafanyabiashara
kudai fidia kwa mali zao zilizoharibika.
Sio wanajeshi pekee waliotuhumiwa kwa uporaji,
kwani polisi mmoja naye alifikishwa mahakamani kwa kosa la uporaji baada ya
kupatikana na pochi la mtu liliokuwa na damu.
Wanagambao wa Al Shabaab
waliteka nyara jengo la Westgate kwa siku nne na kusababisha vifo vya watu 60
pamoja na kuwajeruhi zaidi ya watu mia moja
No comments:
Post a Comment
Ahsante kwa Maoni yako