Sunday, 20 October 2013

JULIUS NYAISANGAH "UNCLE J" AFARIKI DUNIA LEO ASUBUHI

Marehemu Julius Nyaisangah akiwa China katika moja ya safari zake za Uandishi wa Habari
Marehemu Julius Nyaisangah akiwa na baadhi ya waandishi wa Habari Mkoani Morogoro
Marehemu Julius Nyaisangah enzi za uhai wake akiwa na waandishi wa Habari wa Ipp Media (ITV na Radio One)
Marehemu Julius Nyaisangah akitambulishwa kwenye moja za Bendi mkoani Morogoro
Marehemu Julius Nyaisangah (wa kwanza kulia aliyekaa) akiwa na waandishi wenzake akiwemo rafiki yake wa karibu Charles Hillary wa Kwanza Kulia waliokaa
Marehemu Julius Nyaisangah akiwa kwenye msiba wa Mfanyakazi wake (Marehemu Titus Munga) Morogoro
Marehemu Julius Nyaisangah
Marehemu Julius Nyaisangah akitunukiwa cheti na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bwana Joel Bendera wengine ni viongozi wa MOROPC (Mwenyekiti Msuya, Katibu Mtendaji Abeid Dogoli)
Marehemu Julius Nyaisangah akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Joel Bendera katika msiba wa aliyekuwa Mhariri wa Michezo wa Abood Television (Titus Munga)
Marehemu Julius Nyaisangah (wa kwanza kushoto) akiwapa maelezo warembo wa Kanda ya Mashariki mwaka jana ndani ya Kituo cha Abood redio
Marehemu Julius Nyaisangah akiwa na mmoja wa watangazaji Mike Mhagama katika studio za Radio One
Marehemu Julius Nyaisangah akilisakata rumba mkoani Morogoro kwenye moja ya hafla mkoani humo
Marehemu Julius Nyaisangah akiwa na rafiki yake Abubakar Liongo pamoja na Othuman Michuzi nje ya Jengo la Abood Media alikokuwa anafanya kazi Nyaisangah kama Meneja Mkuu
Pacha wake Marehemu Julius Nyaisangah, Charles Hillary akiwa kwenye moja ya majukumu yake ya kazi
Marehemu Julius Nyaisangah (Kulia) akiwa kwenye Msiba wa Mhariri wa Michezo wa Abood Media(Titus Munga) kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera na Mstahiki meya wa Morogoro Amir Nondo.
Mungu alikupenda zaidi Mkongwe wa Tasnia ya Habari Nchini Tanzania toka Radio Tanzania (RTD) uliyetoka na Mapacha wenzako Charles Hillary mkahamia Radio One kisha Mkatawanjika mwenzako akaenda BBC wewe ukaja Abood Media kama Meneja Mkuu wa Tv na Radio.
Baada ya kuumwa muda mrefu ukapata nafuu ila jana jioni ukazidiwa tena na kupelekwa Hospital ya mazimbu ambapo umetutoka leo asubuhi.
Mungu akulaze mahali pema peponi
"UNCLE JAY" JULIUS NYAISANGAH

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako