Tuesday 8 October 2013

BUI BUI AACHIA TRACK MPYA - KICHICHI MAWE


Leo napenda kuwapa wimbo wangu mpya unaoitwa hii ngoma. Hii ngoma ni wimbo niliouwimba kwa hisia kali sana kwa lengo la kuongeza juhudi zaidi na kufanya kazi zangu kuwa za kimataifa zaidi.
Ndugu zangu, marafiki zangu na watu wote kwa ujumla, nashukuru sana kwa saport yenu mnayonipa zikiwemo idea za kitanzania hasa Radio, Runinga, Magazeti na kwenye mitandao tofauti tofauti ya kijamii. Ahsanteni sana na msife moyo kwa nguvu zenu, naona kazi zangu zinaendelea kua juu na inatia moyo kwa kweli
Kichichi mawe ni aina ya mchezo mpya wa kucheza na ni njia pia ya kupongezana kama sisi vijana kwa kila jambo linalofanyika, Chichi mawe ni jina la bondia wa ngumi Tanzania anaejulikana sana kwa jina la Franc Miyayusho.
Hivi karibuni Franc amekua akishinda mapambano yake yote na hana historia ya kupigwa hata mara moja. Kwa kuliona hilo mimi kama Buibui na ni msanii wa mziki huu wa nyumbani nimeona bora nimpongeza rafiki yangu mpendwa kwa kutoa aina ya uchezaji inayoitwa kichichi mawe.
Kichichi mawe nitakua nacheza kila nitakapokuwa kwenye show zangu na nitakua nacheza pia kwenye ngoma hii na nipo kwenye maandalizi ya mwisho ya Video yake na nitaonesha jinsi ya uchezaji huo mpya nilioupa jina la KICHICHI MAWE.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako