Sunday 12 January 2014

WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA ISRAEL, ARIEL SHARON AFARIKI DUNIA


Aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani wa Israel, Ariel Sharon, amefariki dunia.
Bwana Sharon amekuwa hali hali mahututi kwa miaka nane akiwa anatumia mamshine kupumua.
Amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 85 baada ya kuugua kiharusi toka mwaka 2006 wakati akiwa kwenye zama za juu za maisha yake ya kisiasa.
Hali yake ilizidi kuzorota katika siku za karibuni na kufanya baadhi ya viungo vyake kushindwa kufanya kazi ikiwemo Figo zake.
Bwana Sharon ni mtu muhimu kwenye historia ya taifa la Israel tangu akiwa jenerali wa jeshi na baadaye mwanasiasa.
Alikuwa kiongozi shupavu lakini atasalia kukumbukwa kwa utata wake mkubwa hasa miongoni mwa wapalestina.
Mkuu wa kituo cha matibabu cha Sheba karibu na mji wa Tel Aviv alisema kuwa Sharon alifariki Jumamosi jioni.
Rais Shimon Peres alisema kuwa Sharon aliijenga Israel ingawa afisaa mmoja mkuu akaongeza kuwa safari ya Sharon ilikuwa ya vita na mashambuliika ili kuweza kufikia malengo yake ya kisiasa.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako