Sunday 12 January 2014

MAADHIMISHO MIAKA 50 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR


Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar hii leo inaadhimisha kumbukumbu ya miaka hamsini ya mapinduzi ambayo kwenye historia yanaonyesha yaliyomaliza utawala wa Kisultani visiwani humo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameongoza sherehe hizo ambazo pia zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka Tanzania bara akiwemo rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Jakaya Mrisho Kikwete na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal.
Miongoni mwa marais mbali mbali waliohudhuria sherehe hizo ni pamoja na rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni.
Rais Shein amewataka wananchi kuonesha umoja na mshikamano walionao katika sherehe hizo za miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar zinazofanyika kwenye viwanja vya Amani Mjini Unguja.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako