Sunday 12 January 2014

ROBERTO CARLOS ALIPOKUTANA NA TIMU YA YANGA


Beki wa kushoto wa zamani wa Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil Robert Carlos jana amekutana na wachezaji na viongozi wa Yanga kabla ya mazoezi.
Carlos ambaye kwa sasa ni kocha wa timu ya Sivasspor iliyopo Ligi Kuu nchini Uturuki.
Yanga pamoja na Sivasspor zimeweka kambi kwenye hotel ya Sueno Beach zikijiandaa na mashindano mbali mbali yanayozikabili timu hizo.
Yanga wakiwa wameweka kambi kujiandaa na raundi ya pili ya ligi kuu ya Vodacom wenzao Sivasspor wanajiandaa na mchezo kombe la chama cha soka nchini humo ambao utachezwa siku ya jumanne.

No comments:

Post a Comment

Ahsante kwa Maoni yako